12 Kutoka huko tukaende lea na safari hadi Filipi, mji mkuu wa Makedonia ambao ni koloni la Kirumi. 13 Tulikaa Filipi kwa siku chache na siku ya sabato tukaenda nje ya mji kando ya mto, mahali ambapo tulidhani pange faa kwa maombi. Tukakaa chini tukaongea na baadhi ya wanawake waliokuja pale mtoni. 14 Mmoja wa wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mwenyeji wa mji wa Thiatira na mfanya biashara wa nguo za zambarau. Yeye alimpenda Mungu na Bwana akaufungua moyo wake akapokea mahubiri ya Paulo.

Read full chapter